27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

ALIVYOKAMATWA ALIYEJIUNGANISHIA BOMBA LA MAFUTA

Na LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM


JESHI la Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kutoboa na kujiunganishia bomba la mafuta ya dizeli la Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

Watu hao wanatuhumiwa kutoboa bomba la mafuta ya dizeli la Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) na kujiunganishia kwenye matanki mawili yaliyopo ndani ya nyumba yake iliyopo Kisiwani Kigamboni jijini hapa.

Akizungumza na jana, Kaimu Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Benedict Kitalika, alisema usiku wa kuamkia jana walipata taarifa ya Samwel Kitalika kujiunganishia bomba la TPA kwa njia ya kuchomelea na kuunganisha hadi kwenye matanki yake mawili yaliyochimbiwa chini ndani ya nyumba yake.

“Hadi sasa hivi bado askari wako eneo la tukio wanaendelea na uchunguzi, tayari watu wengine wanne wanashikiliwa, hivyo jumla ya waliokamatwa ni watano” alisema Kitalika.

Alisema mtuhumiwa alijiunganishia katikati na bomba kuu hivyo mafuta yanapopelekwa sehemu husika mengine yanaingia kwake hivyo hayafiki kama yalivyokusudiwa.

“Mafuta yanaweza yakapelekwa lita 4,000 sehemu husika lakini hayafiki yote mengine yanaenda kwa mtuhumiwa huyu matokeo yake wanajiuliza haya mengine yameenda wapi,” alisema Kamanda Kitalika

Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi cha Polisi Bandari, Robert Mayalla alisema inavyoonekana huyu mtuhumiwa alijiunganishia kipindi mabomba hayo yanajengwa kwa kuwa kipindi hiki isingewezekana.

Alisema bomba hilo amejiunganisha kwa utaalamu wa juu kwa kuwa hayo mabomba yamepitishwa chini ya ardhi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles