33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

ZIFAHAMU MBINU BORA KATIKA MALEZI

NA DK. CHRIS MAUKI


MALEZI yawezekana kutolewa kwa watoto wetu au ndugu zetu au hata watoto wa wenzetu. Hakuna mzazi au mlezi mwenyekusudi au atakayefurahia kuona mtoto wake anaharibika kimalezi, kila mmoja anahamu ya kuona yale anayoyatamani kwa mtoto au watoto wake yanatimia, ikiwemo malezi mazuri, heshima, elimu bora, kazi bora na hata kupata familia bora.

Kila mzazi au mlezi anakiu na ndoto ya kuona anamuandaa mtoto wake kuwa baba bora au mama bora katika familia yake ya kesho.  Jambo lolote linalotokea na kuonekana kutaka kuharibu ndoto au maono haya ya mzazi huumiza sana moyo wa mzazi na hata kumkatisha tamaa.  Hii imepelekea mahusiano ya baadhi ya watoto na wazazi wao kufa au kulegalega, watoto wengine wametengwa au kufukuzwa majumbani mwao nk.

Kati ya vitu vinavyoharibu mahusiano ya wazazi na watoto wao, na kuwakatisha tamaa kabisa wazazi ni baadhi ya tabia kama vile, utovu wa nidhamu, kujiingiza katika mapenzi, kupata mimba au kumpa msichana mimba, ulevi, uvutaji wa sigara, bangi au madawa ya kulevya, magomvi, utoro wa shule, uvivu na mengine mengi.

Jinsi miaka inavozidi kwenda na jamii inavyozidi kubadilika ndivyo kazi ya malezi inavyoonekana kuwa ngumu zaidi, kila mzazi analalamika kuwa watoto wakuwa mzigo mkubwa unaoshindikana kubeba mara nyingine.

Kwa uzoefu kama mshauri wa kisaikolojia nina kesi tele za watoto walioshindikana na wale wenye tabia zinazosumbua wazazi au walezi wao, hii inaonyesha kuwa tatizo hili ni dhahiri.  Tofauti kubwa na miaka ya nyuma wakati wazazi wetu wanakua na kusoma maisha yalikuwa tofauti. Sasa hivi dunia inabadilika kwa kasi kila siku, vyanzo vya taarifa vinaongezeka, vikitoa taarifa nzuri na mbaya, wakati huhuo wazazi hawataki kubadilika, wakiwa na mawazo ya zamani na kulinganisha enzi zao na enzi hizi, wengi wakionekana kushangaa tafauti wazionazo baina ya vizazi hivi viwili.

Wazazi wengi bado wanaona aibu kuwa wazi  kutoa baadhi ya taarifa na msimamo yao kwa watoto wao wakidhani kuwa muda bado, na ni aibu kufanya hivyo mapema, kumbe jinsi wanavyochelewa ndivyo jinsi ulimwengu unawapa taarifa  potofu juu ya vitu kama mahusiano, mapenzi, ngono, ukimwi na magonjwa ya zinaa nakadhalika.

Mambo haya mengi na tofauti hizi nyingi zinachangiwa na jinsi watoto hawa wanayolelewa na mbinu za malezi ambazo wazazi wamekuwa wakizitumia.  Mara nyingi nimekuwa nikisema kuwa suala si mzazi au wazazi kulazimisha watoto kuwa na nidhamu, suala ni njia au mbinu gani za kujenga nidhamu zinatumika.  Wengi wamewaharibu watoto wao wenyewe pasipo kujua na wakati huo wao wakidhani wanawajenga na kuwaadabisha.

Mtiririko huu wa aina za malezi utakusadia kujitambua na ikiwezekana kubadilika, kama wewe ni mlezi sasa itakusaidia kubadilisha mtazamo wako kuhusu malezi na kama sio mlezi basi itakuandaa vema kwa mlezi bora baadae.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles