27.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 21, 2024

Contact us: [email protected]

Zidane: Nimetimiza malengo yangu

Zinedine ZidaneMADRID, HISPANIA

KOCHA wa klabu ya Real Madrid, Zinedine Zidane, amesema ametimiza malengo yake baada ya kuchukua taji la Ligi ya Mabingwa juzi.

Kocha huyo amefanikiwa kutwaa taji hilo ikiwa ni miezi mitano tangu ateuliwe kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo huku akichukua nafasi ya Rafael Banitez.

Timu hiyo juzi ilichukua ubingwa huo baada ya kuwafunga wapinzani wake Atletico Madrid mabao 5-3 kwa mikwaju ya penati baada ya kumalizika dakika 120 kwa sare ya 1-1, hivyo Zidane amesema ametimiza lengo lake kubwa.

“Nina furaha kubwa kwa kile nilichokifanya tangu nimechaguliwa kuwa kocha mkuu wa klabu hii, ninaamini kila kocha anakuwa na lengo la kutwaa taji hilo kubwa duniani, furaha yangu ni kwamba nimeanza na kufanikiwa kutwaa.

“Haikuwa kazi raisi kuchukua ubingwa huo, kuna wakati ulikuwa mgumu lakini niliweza kupambana hadi kufika hapa, napenda kuwashukuru wachezaji wote, viongozi wa timu na mashabiki kwa ushirikiano waliouonesha,” alisema Zidane

Kwa upande wa kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone, amesema kwamba timu yake ilizidiwa uwezo kila idara na walishindwa kutumia nafasi walizopata.

“Real Madrid ina kikosi cha wachezaji bora, wenzetu walikuwa na uwezo mkubwa zaidi yetu, lakini nasi tulikosa umakini kwa kuwa tulipata nafasi nyingi za wazi ila tulishindwa kuzitumia,” alisema Simeone.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles