28 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

Karrueche atamani kurudiana na Chris Brown

Chris-Brown-and-Karrueche-TranNEW YORK, MARAKENI

MWANAMITINDO maarufu nchini Marekani Karrueche Tran, amesema kwamba anatamani kurudiana na aliyekuwa mchumba wake mkali wa muziki wa RnB, Chris Brown.

Mrembo huyo tangu ameachana na Brown amekuwa kimya kuzungumzia uhusiano wao, lakini juzi kupitia akaunti yake ya Instagram aliweka picha ya msanii huyo na kuandika kwamba anatamani siku zingerudi nyuma ili aendelee kuwa naye.

Hata hivyo walivyoachana mwanzoni mwa mwaka huu, mrembo huyo aliwahi kusema kwamba yupo tayari kurudiana na msanii huyo kama atakuwa tayari na hatojali yaliyotokea.

“Bila ya kujali nini kimetokea katika uhusiano wetu, lakini nitakuwa tayari kumpokea Chris muda wowote akiwa tayari kuwa na mimi tena,” aliwahi kusema mrembo huyo.

Hata hivyo tangu wawili hao waachane Chris hajaonekana akiwa na mrembo mwingine, lakini Karrueche alionekana akiwa na mchezaji wa Manchester United, Memphy Depay.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles