22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Simeone afikiria kuongeza mkataba mpya

Diego SimeoneMADRID, HISPANIA

KOCHA wa klabu ya Atletico Madrid, Diego Simeone, amesema baada ya kumaliza fainali ya Ligi ya Mabingwa sasa anafikiria kuongeza mkataba mpya katika klabu hiyo.

Simeone amesema amekuwa na miaka mitatu ya kuikumbuka katika klabu hiyo, hivyo baada ya kumalizika kwa fainali ya Ligi ya Mabingwa anaweza kuzungumza na waajiri wake kwa ajili ya mkataba mpya.

“Tumemaliza Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Ulaya, hapa sasa naweza kufanya mazungumzo na viongozi wa klabu yangu kuona kama kuna uwezekano wa kuongeza mkataba au kutafuta klabu nyingine, lakini bado nina mapenzi na klabu hii kutokana na ushirikiano ninaoupata,” alisema Simeone.

Kocha huyo aliongeza kwa kusema kwamba, ameumizwa na matokeo yake katika mchezo wa fainali dhidi ya wapinzani wao Real Madrid.

“Fainali ya mwaka huu imenigusa zaidi kwa kuwa niliamini naweza kuwa bingwa na wengi waliamini hilo, lakini matokeo yamekuwa tofauti na matarajio ya wengi, kikubwa ninachokifikiria ni wale ambao walijitokeza katika mchezo huo kwa ajili ya kuipa nguvu timu yao, ila waendelee na hali hiyo kwa misimu mingine,” aliongeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles