29.9 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Zawadi NT aachia video ya Number One

Na Mwandishi Wetu

Msanii kutoka Australia, Zawadi NT anayefanya vizuri kwenye muziki wa Injili, ameachia video ya wimbo wake mpya unaoitwa, Number One ukiwa ni wimbo wake wa kwanza kwa mwaka 2021.

Zawadi amesema wimbo huo umebeba ujumbe wa kumsifu Mungu na kuihamasisha jamii kumuweka Mungu katika nafasi ya kwanza kwenye kila kitu.

“Katika kila hali Yesu ni shujaa wako namba moja, hivyo huu ni wimbo wa kumsifu Mungu na unaweza kuchezeka kiasi kwamba ukatumika kwenye sherehe mbalimbali kama harusi, video imeshatoka ipo kwenye chaneli yangu ya YouTube kila mtu anaweza kuitazama na kubarikiwa,” alisema mwimbaji huyo mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Aidha, Zawadi ameongeza kuwa wimbo, Number One unapatikana kwenye mitandao yote ya kusikiliza na kuuza muziki duniani ambapo shabiki wake anaweza kuupata huko kwa urahisi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles