27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

TACAIDS yaombwa kutoa elimu kwa makundi maalum

Na Faraja Masinde, Dar es Salaam

Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi(TACAIDS) imeombwa kutoa elimu zaidi ya Ukimwi kwa makundi maalum ikiwemo kutumia wakalimani wa lugha.

Wito huo umetolewa leo Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Chama Cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) mkoa wa Dar es Salaam, Habibu Mrope kwenye semina ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa watu wenye ulemavu wa kusikia (Viziwi) Mkoa wa Dar es Salaam.

“Ni kweli kwamba tume ya kudhibiti ukimwi imekuwa ikifanyakazi nzuri ya kuelimisha umma kwenye mambo mbalimbali yakiwamo ya maambuzi lakini bado kuna changamoto kwa makundi maalumu katika kufikiwa na elimu hii.

Washiriki wa semina hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya mafunzo hayo kufunguliwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ACAIDS, Jumanne Isango.

“Mfano ukiangalia kwenye matangazo mbalimbali ambayo mmekuwa mkiyatoa kwenye vyombo vya habario bado ni changamoto kwetu kuweza kuelewa kwamba yanazungumzia nini kutokana na kutokuwa na mkalimani wa lugha.

“Hivyo ni muhimu jambo hilo likapewa mkazo kwani kama tunavyofahamu kwamba sisi ndio tuliko kwenye hatari kubwa ya maambuzi na ndiyo maana utakuta tukiambukizwa kwani ni rahisi kulaghaiwa,” amesema Mrope.

Mrope amesema makundi hayo maalumu yamekuwa yakidanganywa kutokana na kutokupata taarifa sahihi hatua ambayo inachangiwa na kukosekana kwa wakalimani.

Aidha, Mrope amesema iwapo taarifa na matangazo mbalimbali ya serikali yanayorushwa kwenye vyombo vya habari yatawalenga na watu wenye ulemavu kwa kuwa na lugha ya alama, yatachangia kwa kiuasi kikubwa elimu kufika kwenye makundi hayo kinyume na ilivyo hivi sasa.

Upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Tacaids, Jumanne Isango akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, Dk. Loenard Maboko, amesema wamepokea changamoto hiyo na kwamba wataufanyia kazi katika kuhakikisha kuwa elimu inayafikia makundi hayo yote.

“Huu ni mwendelezo wa Tacaids katika kuhakikisha kwamba tunayafikia makundi yote maalum nchini lengo likiwa ni kupunguza kabisa maambukizi mapya ya ukimwi.

“Tunajua changamoto mnayoipata ikiwamo kufikiwa na elimu ambapo hata matangazo tunayoyatoa yamekuwa siyo rafiki kwenu ikiwamo yale ya Redio na Televisheni kutokana na kutokuwa na Wakalimani, lakini niwaahidi kuwa kupitia idara husika tutajitadi kuhakikisha kwamba tunalifanyia kazi hilo na kutoa kipaumbele kwa makundi maalumu likiwemo la viziwi ili kufikia Tanzania isiyo na unyanyapaa pamoja na maambukizi ya ukimwi kama ambavyo tunasema kwamba hakuna mtu kuachwa  nyuma,” amesema Isango na kuongeza kuwa:

“Niseme tu kwamba serikali tumejipanga kuweza kuzifanyia kazi changamoto hizi ikiwamo kuongeza mafunzo ya watu wanaofanyakazi ya ukalimani ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya wahusika kwani mbali na masuala ya Ukimwi pia wanatakiwa kutumika kwenye nyanja mbalimbali.

“Kwani kuna watu ambao hawaoni, hawasikii na aina nyingine za ulemavu hivyo lazima tutoe elimu,” amesema Isango.

Aidha, ametoa wito kwa wadau wengine wote kuhakikisha kuwa suala la kuwashirikisha wakalimani linapewa kipaumbele kwa manufaa ya watu wenye ulemavu.

“Pia kwenye utoaji wa takwimu watu wenye ulemavu watajwe kwa namna yao ya pekee na siyo tutoa tu kiujumla,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles