ZARI AMPONGEZA DIAMOND KWA OFISI MPYA

0
1133

NA CHRISTOPHER MSEKENA

NYOTA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, juzi alionyesha mjengo wa ghorofa moja utakaotumika kama ofisi mpya za Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) unaopatikana maeneo ya Mbezi Beach, Dar es Salaam.

Mpenzi wake, Zari amemsifia kwa kile anachokifanya kwa kujituma kiasi cha kufungua kituo cha redio na runinga kwa kusema: “Hongera sana Diamond kwa juhudi na bidii uliyonayo, Allaah akujalie kwa mengine mazuri zaidi. Siku zote umekuwa mpiganaji wa kazi zako, kwa kuwa njia pekee ya kuijenga familia ni kupiga kazi, najua malengo yako Alhamdulillah!”

Ndani ya jengo hilo lenye thamani ya shilingi Bilioni 1 litakalozinduliwa Februari Pili, mwaka huu kutakuwa na studio za kurekodi muziki, studio za picha na filamu, wafasi.com na studio za redio na runinga (Wasafi Fm, Wasafi Tv).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here