24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

Z ANTO KUWASHANGAZA MASHABIKI

Na GLORY MLAY

MWIMBAJI wa muziki wa Bongo Fleva  aliyewahi kufanya vizuri na wimbo wake wa Binti Kiziwi, Ally Mohammed ‘Z Anto’, amesema kwa mwaka huu mpya anatarajia kuachia audio na video zake mpya tatu kwa ajili ya ‘kuwasuprise’  mashabiki wake.

Msanii huyo alisema anataka kupunguza ukimya alionao katika muziki, hivyo yupo katika maandalizi ya kuachia audio na video hizo tatu.

“Mungu akijalia kuanzia mwaka huu mpya ninatarajia kuachia audio na video zangu tatu ambazo zipo jikoni na muda wowote nitaanza kuachia moja moja, nimekaa kimya kwa muda kidogo nikitafakari nifanye nini ili niweze kuwarudisha mashabiki wangu kwenye mstari, sasa ninakuja na kazi hizo,” alisema.

Msanii huyo aliongeza kwa kuwataka mashabiki wake waendelee kusubiri kazi hizo ambazo zimefanywa kwa ubora wa hali ya juu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles