MSAGA SUMU KUFUNGUA MWAKA NA RAIS MSTAAFU

0
1116

Na GLORY MLAY

BAADA ya kufanya vizuri na ngoma yake ya ‘Mwanaume Mashine’, hatimaye Mfalme wa muziki wa Singeli nchini Tanzania, Selemani Jabiri ‘Msaga Sumu’, anatarajia kuachia ngoma yake ya kufungua mwaka ijulikanayo kwa jina la Rais Mstaafu.

Akizungumza na MTANZANIA, Msaga Sumu alisema hiyo itakuwa zawadi tosha ya mwaka mpya kwa mashabiki zake ambao wamekuwa bega kwa bega katika kipindi chote cha mwaka 2017.

“Nawapenda sana mashabiki zangu kwa kuwa wamekuwa msaada kwangu, hawajawahi kuniacha hata wakati wa shida, hivyo nitawapa zawadi ambayo itakuwa maalumu kwao kwa mwaka mpya wa 2018,” alisema.

Msanii huyo amewataka wasanii wenzake kuhakikisha wanafanya makubwa 2018 ili kutimiza malengo yao ambayo hayakufanikiwa mwaka 2017.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here