Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital
Klabu ya Yanga kwa asilimia kubwa imemaliza kutengeneza kikosi chake cha msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya leo Ijumaa Agosti 13, kutambulisha wachezaji wawili wa Kimataifa walikuwa wanasubiriwa na mashabiki wa Wanajangwani hao.
Wachezaji hao ni beki Shaaban Djuma na winga Jesus Moloko anayeziba pengo la Tuisila Kisinda, wote raia wa DR Congo wakitokea AS Vita ya nchini humo.
Tofauti na hao, jana Yanga ilimtambulisha beki wa pembeni, David Brayson kutoka KMC, hiyo kufikisha idadi ya wachezaji wapya
Wengine ni Khalid Aucho(Uganda), Heritier Makambo, Fiston Mayele(DR Congo), Djigui Diarra(Mali), wazawa ni Erick Johora, Athuman na Dickson Ambundo.
Wachezaji ambao wamemaliza mikataba na kuachwa rasmi ni makipa wawili Metacha Mnata na Farouk Shikalo, huku Said Makapu naye akiaga mashabiki.