27.9 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Aweso afanya maamuzi magumu baada ya kupokelewa na ndoo za maji Rorya

Na Mwandishi Wetu, Rorya

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso, amepokelewa na kina mama wenye ndoo za maji vichwani wilayani Rorya wakishinikiza upatikanaji wa maji wilayani humo.

Tukio hilo limetokea leo Ijumaa Agosti 13, wakati Waziri Aweso alipotembelea mradi wa Maji Nyarombo, katika wilaya ya Rorya iliyopo mkoani Mara.

Baadhi ya wakazi wa Nyarombo wakifurahia baada ya kuhakikishiwa upatikanaji wa maji na Waziri Juma Aweso.

Akiwa katika eneo la mradi wa maji, Waziri Aweso amemugiza Mkandarasi Gaimo Construction Ltd, anayetekeleza ujenzi wa miundombinu ya mradi huo wa maji kufikisha maji katika tanki la mradi ili wananchi wapate huduma ya majisafi na salama ndani siku saba.

Hatua hiyo imeonekana kuwafurahisha wananchi hao ambapo hawakusita kuonyesha furaha yao wakiamini changamoto yao ya maji ya muda mrefu inakwenda kumalizika.

Katika hatua nyingine, Waziri Aweso amemuelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Anthony Sanga, kutoa  Sh milioni 80 kwa ajili ya kuilipa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), ili waunganishe umeme kwenye mradi huo huku akielekeza zaidi Sh milioni 150 kupeleka maji katika Kitongoji cha Siko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles