23.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Yanga yafunga kazi usajili

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Klabu ya Yanga kwa asilimia kubwa imemaliza kutengeneza kikosi chake cha msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya leo Ijumaa Agosti 13, kutambulisha wachezaji wawili wa Kimataifa walikuwa wanasubiriwa na mashabiki wa Wanajangwani hao.

Wachezaji hao ni beki Shaaban Djuma na winga Jesus Moloko anayeziba pengo la Tuisila Kisinda, wote raia wa DR Congo wakitokea AS Vita ya nchini humo.

Tofauti na hao, jana Yanga ilimtambulisha beki wa pembeni, David Brayson kutoka KMC, hiyo kufikisha idadi ya wachezaji wapya

Wengine ni Khalid Aucho(Uganda), Heritier Makambo, Fiston Mayele(DR Congo), Djigui Diarra(Mali), wazawa ni Erick Johora, Athuman na Dickson Ambundo.

Wachezaji ambao  wamemaliza mikataba na kuachwa rasmi ni makipa wawili Metacha Mnata na Farouk Shikalo, huku Said Makapu naye akiaga mashabiki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles