24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga ‘simple’ kileleni

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

TIMU ya soka ya Yanga, leo itakuwa na kazi rahisi kupaa tena kileleni itakaposhuka dimbani kuivaa Majimaji FC katika mchezo wa kukamilisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo, wanachuana vikali na wapinzani wao Azam FC ambao jana waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Mgambo Shooting katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Matokeo ya ushindi wa jana, yameiwezesha Azam kurejea kileleni na kuishusha Yanga baada ya kufikisha pointi 39 huku ikiwaacha wapinzani wao nafasi pili wakiwa na pointi 36.

Kikosi cha Yanga kinachonolewa na kocha Mholanzi, Hans van der Pulijm, kitaingia uwanjani huku kikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi mwembamba wa bao 1-0 iliyopata katika mchezo wake uliopita dhidi ya Ndanda FC.

Wanajangwani hao watakuwa na kazi moja tu ya kuhakikisha wanaibuka na ushindi mbele ya Majimaji ili kulinda heshima yao Ligi Kuu ya kutofungwa mchezo hata mmoja tangu kuanza kwa ligi hiyo ambapo tayari wamecheza mechi 14 na kushinda mara 11 na kupata sare tatu.

Wapinzani wa Yanga, Majimaji walifanikiwa kupanda daraja msimu huu na kurejea Ligi Kuu ambapo leo watakutana tena na Yanga baada ya kupita kwa misimu kadhaa tangu iliposhuka mwaka 2005.

Kwa mara ya mwisho Yanga ilipokutana na Majimaji jijini Dar es Salaam kabla ya kushuka daraja iliichapa mabao 4-0.

Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Mwadui FC iliyojikusanyia pointi 22 baada ya kucheza michezo 14, itawakaribisha vibonde Kagera Sugar katika Uwanja wa Mwadui, Shinyanga.

Vibonde wengine wa ligi hiyo, African Sports wanaoburuza mkia watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Mtibwa inayoshika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi, inakabiliwa na kibarua kigumu cha kusaka ushindi ugenini ili iweze kuendeleza kasi yake ya kuifukuzia Simba nafasi ya tatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles