23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga roho kwatu

MOHAMMED KASSARE-DAR ES SALAAM

TIMU ya Yanga imeonja radha ya ushindi, baada ya jana  kuilaza Coastal Union bao 1-0, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa Uwanja wa Uhuru,  Dar es Salaam.

Ushindi huo ni wa kwanza msimu huu kwa timu hiyo yenye makao yake makuu, Mitaa ya Twiga na Jangwani jijini hapa.

Yanga ilizindua kampeni zake za ligi hiyo kwa kuchapwa bao 1-0 na Ruvu Shooting kabla ya kulazimishwa sare ya mabao 3-3 na Polisi Tanzania, michezo yote ikipigwa kwenye uwanja huo huo.

Kiungo Abdulazizi Makame aliifungia Yanga bao pekee dakika ya 51 kwa kichwa, akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Mrisho Ngasa.

Mchezo huo ulianza kwa kasi kwa timu zote kushambuliana.

Dakika ya 13, mshambuliaji David Molinga alilishindwa kutumia vema nafasi aliyopata kuiandikia Yanga bao la kuongoza, baada ya mpira wa kichwa aliopiga akiunganisha krosi safi uya beki Juma Abdul kupaa juu ya lango la Coastal.

Dakika ya 31 Menzi Chilli wa Coastal Union alilimwa kadi ya njano kwa kumfanyia madhambi Mapinduzi Balama.

Yanga iliendeleza mashambulizi langoni mwa Coastal Union,  dakika ya 40, mpira wa kichwa uliopigwa na Mapinduzi akiunganisha krosi ya iliyochongwa na Abdul ulitoka nje ya lango la Coastal.

Kipindi cha kwanza kilimalizika huku timu hizo zikiwa nguvu sawa kutokana na nyavu za kila mmoja kutofunguka.

Yanga iliingia uwanjani na nguvu zaidi kipindi cha pili na kufanikiwa kupata bao dakika ya 51 kupitia Makame.

Coastal Union ilifanya mabadiliko dakika ya 57, alitoka Haji Ugando na nafasi yake kuchukuliwa na Hamis Kanduru.

Dakika ya 70, kipa Sudy Abdalah wa Coastal Union alionesha umahiri mkubwa baada ya kuokoa kwa miguu kiki ya Ngassa  wakiwa wanaangaliana.

Ngassa kabla ya kumfikia Abdalah aliwazidi kasi mabeki wa Coastal Union.

Dakika ya 72,  Yanga ilifanya mabadiliko, alitoka  Deus Kaseke na kuingia Japhary Mohammed huku dakika ya 80 akitoka Kelvin Yondan na kuingia Moustafa Seleman.

Dakika ya 85,  Feisal Salum ‘Fei Toto’ alilimwa kadi ya njano kwa kumchezesha  rafu Ayoub Semtawa.

Dakika 90 zilikamilika kwa Yanga kutoka kifua mbele kwa ushindi wa bao 1-0.

Yanga: Farouk Shikalo, Juma Abdul, Ally Mtoni, Ally Ally, Kelvin Yondani, Feisal Salum, Mrisho Ngasa, Abdulaziz Makame, David Molinga, Mapinduzi Balama na Deus Kaseke.

Coastal Union: Soud Abdallah, Hassan Kibalo, Omary Salum, Stanley Kenedy, Bakari Nondo, Mtenje Albano, Haji Ugando, Ayoub Semtewa,  Shaban Idd, Menzi Chilli na Ayoub Lyanga

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles