28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Mahakama yamuachia kinara wa upinzani

YOUNDE, CAMEROON

Mahakama ya Kijeshi ya Cameroon imemuachia huru kiongozi wa upinzani nchini humo Maurice Kamto, kufuatia agizo lililotolewa na Rais Paul Biya.

Rais Biya ametoa amri ya kufutwa mashitaka yote yaliyokuwa yakimkabili mwanasiasa huyo wa upinzani.

Waziri Mkuu wa Cameroon, Joseph Dion Ngute Alisema jana kuwa kwa mujibu wa Katiba, Rais wa Jamhuri, anayo haki ya kusimamisha kesi ikiwa anaona kuwa kusitishwa kwa kesi hiyo kuna faida kubwa kwa maslahi ya taifa.

Awali, Rais Biya aliamuru pia kuachiliwa huru kwa wafungwa 333 wanaotuhumiwa kuhusika na mgogoro uliozuka katika maeneo yanayozungumza Kiingereza, wakati mazungumzo ya amani yalipokuwa yakiendelea.

Mazungumzo makubwa ya kusaka amani na kufikia mapatano ya kitaifa kati ya Serikali ya Cameroon na wapinzani wa maeneo yanayozungumza Kiingereza yalimalizika Ijumaa ya Oktoba 4 mjini Yaounde.

Hata hivyo, kuwekwa kizuizini bila kufunguliwa mashtaka kiongozi huyo wa chama cha upinzani cha Renaissance Cameroon, Maurice Kamto na pia kutoshiriki mazungumzo hayo kiongozi mkuu wa Wacameroon wanaopigania kujitenga katika maeneo ya nchi hiyo yanayozungumza Kiingereza ni katika mambo yaliyoyafanya mazungumzo hayo yakose sura na uakilishi wa kitaifa.

Julius Ayuk Tabe, aliyejitangaza kuwa Rais wa Ambazonia anatumikia kifungo cha maisha jela tangu miezi michache iliyopita katika gereza kuu la Yaoundé.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles