25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga Princess, Simba Queens mechi ya kibabe

Na Winfrida Mtoi, Dar es Salaam

Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara utakaopigwa kesho kati ya Yanga Princess na Simba Queens, makocha wa timu hizo, Edna Lema na Mussa Mgosi, wameahidi kutoa burudani ya kuvutia kwa mashabiki wa soka.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Katika mechi ya kwanza ambayo Simba alikuwa mwenyeji, Uwanja wa Mo Simba Arena, Desemba, mwaka jana, timu hizo zilitoka suluhu.

Mchezo wa kesho kila timu inahitaji matokeo ya ushindi kutokana na msimamo wa ligi hiyo ulivyo, Yanga Princess ikiwa kileleni na pointi 38, ikifuatiwa na Simba alama 36 zote zikicheza mechi 14.

Kocha wa Yanga Princess, Edna, amesema wamejiandaa vizuri na kikosi chake kipo fiti kwa mapambani ya kusaka pointi tatu.

Kwa upande wake, Mgosi, amewatoa hofu mashabiki wa kikosi hicho na kuwataka kufika uwanjani kushuhudia burudani ya kuvutia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles