26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Ndejembi awasha moto wanaokata fedha za wanufaika TASAF

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi, amepiga marufuku watendaji wa kata na vijiji ambao wamekua na tabia ya kuwakata fedha za TASAF wanufaika wa mfuko huo ambao ni wale wanaotoka Kaya maskini badala yake amewataka kuzisaidia Kaya hizo kukua kiuchumi. 

Naibu Waziri Ndejembi ametoa agizo hilo akiwa katika Kata ya Dabalo wilayani Chamwino mkoani Dodoma alipofanya ziara ya kikazi katika kata za Membe, Dabalo na Segala ambapo pia amekagua miundombinu ya barabara katika Kata ya Itiso, Ujenzi wa Madarasa katika Shule ya Sekondari Membe na Shule ya Sekondari ya Segala.

Akizungumza katika kikao cha ndani na viongozi wa Kata hizo upande wa Serikali na wale wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndejembi amesema ni marufuku kwa Mtendaji yeyote awe wa Kata au Kijiji kumkata fedha mwananchi ambaye anapokea fedha za mfuko wa TASAF kwani kufanya hivyo ni kuzidi kumdidimiza.

Amesema tayari amepokea malalamiko kutoka sehemu mbalimbali nchini zikiwalalamikia watendaji hao kuwa na tabia ya kuwakata wanufaikaji hao wa TASAF fedha za michango ya shule na miundombinu ya afya ikiwemo Bima ya CHF iliyoboreshwa jambo ambalo linazidi kuzididimiza Kaya hizo badala ya kuzinyanyua.

” Ni marufuku kwa mtendaji yoyote kuwakata wanufaika wa TASAF fedha zao, lengo la Serikali ya Rais Dk John Magufuli ni kuzinyanyua Kaya hizi kutoka kaya maskini hadi kuwa kaya zenye uhakika wa kula, sasa haiwezekani kaya hiyo inapokea Sh 40,000 halafu eti unaikata michango ya shule huko ni kuididimiza na siyo kuisaidia, niwatake watendaji wetu kuwasaidia wananchi hawa badala ya kuwaumiza.

Rais wetu Dk. John Magufuli amekua akihakikisha serikali inapeleka fedha hizi kwa kaya maskini kwa ajili ya kuzikomboa, lengo likiwa kuwanyanyua waweze kupata Bima za CHF wenyewe kama watatumia fedha hizo kufuga au kulima sawa lakini ilimradi wajinyanyue kiuchumi, hivyo sitaki kusikia tena malalamiko hayo ya kukatwa fedha kwa ndugu zetu hao,” Amesema Naibu Waziri Ndejembi.

Amesema kitendo cha kuwakata fedha hizo ambazo wanapatiwa kwa ajili ya kuboresha uchumi wao ni kuzidi kuwadidimiza wananchi hao jambo linaloenda kinyume na Mpango wa serikali wa kuzidi kuzinyanyua kaya hizo maskini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles