22.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

YANGA KULIPA MIL 53/- KESI YA KESSY

kessy

Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) kupitia Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji, imeitaka klabu ya Yanga kulipa jumla ya Sh milioni 53, baada ya kuibaini imekiuka utaratibu katika kumsajili mchezaji, Hassan Ramadhani ‘Kessy’.

Sakata hilo lilichukua takribani miezi sita kabla ya kupatiwa ufumbuzi na Simba kuibuka kidedea.

Ikitangaza uamuzi wake huo jana, kamati hiyo iliyo chini ya Mwenyekiti, Richard Sinamtwa, iliitaka Yanga kulipa Sh milioni tatu kwa kukiuka kanuni ya usajili  ya TFF na Sh milioni 50 kama fidia kwa klabu ya Simba ambayo bado ilikuwa na mkataba na mchezaji huyo.

Taarifa ya kamati hiyo ilifafanua kuwa, hukumu hiyo ilitolewa  baada ya kupitia mawasilisho ya pande zote mbili kwa njia ya mahojiano na vielelezo, kisha kubaini  kasoro kwenye usajili wa Kessy kwenda Yanga.

“ Mchezaji Hassan  Ramadhan ‘Kessy’ alikuwa na mkataba na klabu ya Simba uliokuwa unaisha Juni 15, mwaka huu.

“Yanga walikiri mbele ya kamati kupeleka jina la mchezaji, Hassan Ramadhani Kessy, katika Shirikisho la Soka Barani  Afrika (CAF) Juni 10, mwaka huu, huku mchezaji huyo akiwa ndani ya mkataba na klabu ya Simba,” ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa, TFF kupitia sekretarieti yake ilikuwa na nafasi ya kuielekeza Yanga hatua stahiki za kuchukua, ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Simba kama taratibu zinavyoelekeza.

“Kama hatua hii ingechukuliwa kwa wakati mwafaka, mgogoro huu usingekuwa na sura ya sasa na pengine usingekuwepo.

Kitendo cha Yanga kupeleka jina la mchezaji wa klabu nyingine CAF, huku mchezaji huyo akiwa ndani ya mkataba na mwanachama mwingine wa TFF, ni kosa kubwa kwa mujibu wa kanuni za ligi kifungu 69 (5),” ilifafanua taarifa hiyo.

Ikiendelea kuelezea kuwa kutokana na  kosa hilo, Yanga inapaswa kupewa adhabu itakayotumika kama funzo kwa wanachama wote kuheshimu nafasi ya TFF kwenye suala la usajili badala ya  kwenda CAF au kwingineko, ili kulinda heshima na uadilifu wa soka nchini.

“Ofisa wa TTF aliyehusika ama kwa kushirikiana na uongozi wa klabu ya Yanga au kwa kutochukua hatua stahiki kwa wakati, apelekwe kwenye mamlaka yake ya nidhamu, yaani, Katibu Mkuu wa TFF ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yake.” ilisema taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles