27.9 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga kuivaa JKT Mlale Kombe la FA

kikosi cha yangaNA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga, leo wataingia uwanjani kusaka pointi tatu muhimu dhidi ya JKT Mlale katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la FA, utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga wataikabili JKT Mlale bila kiungo wake mahiri, Haruna Niyonzima, ambaye ni majeruhi kutokana na kuumia goti wakati timu hiyo ilipokutana na mahasimu wao, Simba, Jumamosi iliyopita.

Mchezo huo pia ni sehemu ya maandalizi ya kikosi hicho kuelekea mchezo wao wa kimataifa wa marudiano wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya wapinzani wao, Cercle de Joachim, utakaopigwa Jumamosi hii katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kocha Mkuu wa Yanga Mholanzi, Hans van der Pluijm, aliliambia MTANZANIA jana kuwa kila kitu kinaendelea vizuri kuelekea mchezo huo, huku akielezea kuridhishwa na kiwango cha wachezaji wake ambao watashuka dimbani kuikabili JKT Mlale.

“Kila kitu kinakwenda vizuri kwa upande wetu, hali za wachezaji zinaridhisha, isipokuwa Niyonzima ambaye jana alishindwa kufanya mazoezi kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti,” alisema.

Yanga, ambao walifanikiwa kutinga hatua ya 16 bora baada ya kuichapa Friends Rangers mabao 3-0, wamepania kuendeleza kasi yao ya ushindi kwenye Kombe la FA ili waweze kusonga mbele na kurahisisha kasi ya kutwaa ubingwa.

Katika kuhakikisha anatimiza malengo ya ushindi, Pluijm ameendelea kukiimarisha kikosi chake, hasa katika safu ya ushambuliaji, kwa kuwapa mbinu tofauti za ufungaji wa mabao ya mbali kama alivyofanya wakati wakiwa kambini visiwani Pemba, kujiandaa na mechi ya watani wa jadi waliyoshinda mabao 2-0.

Katika mazoezi hayo yaliyofanyika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam jana, Pluijm alionekana kuongeza umakini kwa kuhakikisha kila mchezaji anafanya vizuri kwa kutendea haki nafasi za kufunga wanazopata, akilenga zaidi ushindi wa mabao mengi.

Washambuliaji wa Yanga waliong’ara mazoezini jana na kuwa kivutio kwa mashabiki waliohudhuria kutokana na kasi yao ni Amissi Tambwe na Malimi Busungu, ambao kila mmoja aliweza kutikisa nyavu kwa kila upande.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles