25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Malinzi akana upangaji matokeo FDL

malinziNA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, amekana kuhusishwa na upangaji wa matokeo ya michezo miwili Ligi Daraja la Kwanza kusaka timu zitakazopanda Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao, kutoka kundi C la ligi hiyo.

Michezo hiyo ilizikutanisha timu ya JKT Kanembwa, ambayo ilipokea kipigo cha mabao 8-0 kutoka kwa Geita Gold katika mechi iliyofanyika Uwanja wa Lake Tanganyika, mjini Kigoma, wakati Polisi Tabora ilishinda mabao 7-0 dhidi ya JKT Oljoro kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, mjini Tabora.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Malinzi alisema anashangazwa kuona habari za yeye kuhusishwa kupanga matokeo na kuonyesha upendeleo wa wazi kwa timu ya Geita Gold na Polisi Tabora.

Malinzi alisema wenye vielelezo na uhakika, wanatakiwa kuwasilisha malalamiko yao Polisi na kuacha kusambaza habari za uongo.

“Nafahamu yote yanayoendelea, nimekaa kimya tu, lakini naona mengi yanazidi kuongelewa na sasa imefikia hatua naambiwa nilisambaza ujumbe mfupi wa simu kwa waamuzi, vizuri wale wote wanaosema nimehusika kupanga matokeo kwa namna moja au nyingine wafike katika vyombo vya sheria, ikiwa wana uhakika na wanachokizungumza.

Rais huyo alieleza, maneno ambayo yanaendelea kusemwa hayatajenga kitu chochote, kwani kwa asilimia kubwa yatachangia soka la Tanzania kurudi nyuma.

Wakati huo huo, Malinzi alisema sakata la tuhuma za upangaji wa matokeo hayo, linatarajiwa kujadiliwa na Kamati ya Nidhamu ya TFF Machi 20, mwaka huu, baada ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa ligi kushindwa kulitolea majibu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles