24.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Wapinzani wa Yanga kutua leo Dar

foot11fev*Waamuzi wa Eritrea kuamua pambano hilo

NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

WAKATI timu ya Yanga ikiendelea kusherehekea ushindi wa bao 2-0 dhidi ya watani wao wa jadi Simba, wapinzani wao katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika, Cercle de Joachim, wanatarajia kutua nchini leo kwa ajili ya mchezo wa marudiano Jumamosi hii utakaochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga iliyopata ushindi mwembamba wa bao 1-0 katika mchezo wa awali uliochezwa ugenini, inatarajia kuchomoza na ushindi pia katika mchezo wa marudiano.

Cercle de Joachim inakutana na Yanga ikiwa ina kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya Riviere du Rempart, kwenye Ligi Kuu ya Mauritius, ambayo ipo nafasi ya saba kwa kujikusanyia pointi 15.

Ushindi huo wa Cercle katika ligi yao, umeifanya kuendelea kuwa kwenye nafasi ya nne ikiwa na pointi 30 baada ya kucheza michezo 17, lakini imebakiwa na michezo miwili mkononi ya viporo, wakati Yanga inakutana nayo ikiwa imeifunga timu ngumu Simba na kupata nafasi ya kurudi kileleni ikiwa na pointi 46.

Cercle inatua nchini ikiwa na rekodi ya kucheza michezo tisa ugenini na kufanikiwa kupata ushindi katika michezo mitatu tu kwenye ligi hiyo, huku  michezo nane ya nyumbani ilishinda  sita.

Kutokana na rekodi hiyo inaonekana kuwa Cercle ni timu dhaifu kwenye michezo ya ugenini kwa kuwa na uwiano wa ushindi wa 0.89, huku Yanga ilikuwa na uwiano wa 2.4 katika michezo ya ugenini.

Timu hiyo inatua na kikosi kamili ambapo hadi sasa kikosi chao hakijaripotiwa kuwa na majeruhi.

Waamuzi watakaochezesha mchezo huo watatoka Eritrea na mwamuzi wa kati atakua Amanuel  Eyob Russo, akisaidiwa na Suleiman Ali Salih na Hugush Abdelkader wakati Kamisaa ni Idrisa Osman.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,093FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles