24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Azam kuishusha Yanga kileleni leo?

kikosi cha azam kagameNA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

KIKOSI cha timu ya soka ya Azam FC leo kitakuwa katika kibarua kigumu ugenini kitakapovaana na wenyeji wao, maafande wa Tanzania Prisons, katika Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Mchezo huo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambao ni wa kiporo, unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua, kutokana na historia ya timu hizo kila zinapokutana.

Mara nyingi Prisons imekuwa ikiutumia vyema uwanja wake wa nyumbani, ambao katika msimu huu iliweza kuichapa Simba bao 1-0 na baadaye kulazimisha sare ya mabao 2-2 na Yanga.

Rekodi ya timu hizo inaonyesha kuwa zimekutana mara 11 katika mechi mbalimbali za ligi, ambapo wametoka sare mara tano, huku kila timu ikifanikiwa kushinda michezo mitatu.

Azam hawajafanikiwa kushinda mechi hata moja wakicheza Uwanja wa Sokoine, kutokana na kufungwa mara mbili na kupata sare tatu, jambo linalowafanya wauchukulie kwa uzito wa hali ya juu mchezo huo ambao utawawezesha kurudi kileleni.

Jumla ya mabao 20 yamefungwa na timu hizo katika mechi zote 11 walizokutana na kila timu imefunga mabao 10, jambo linaloweza kuongeza ushindani kwa kila mmoja kutaka kumzidi mwenzake.

Lakini Azam, waliopania kuwashusha wapinzani wao Yanga kileleni, wataingia uwanjani kwa kujiamini zaidi kutokana na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao 2-2 waliopata katika mchezo wa kwanza dhidi ya Prisons, uliofanyika Uwanja wa Azam Complex.

Katika mchezo uliopita, Azam ilishinda mabao 3-0 dhidi ya Mbeya City kwenye uwanja huo, hali inayoweza kuwaongezea morali ya kutaka kuendeleza wimbi la ushindi na kurejea kileleni.

Akizungumzia mchezo huo, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Stewart Hall, alisema utakuwa mgumu kutokana na ubora wa kikosi cha Prisons, ambacho msimu huu kiwamezidi maarifa Mbeya City.

Alisema wana nafasi ya kupata ushindi kama wachezaji watacheza vizuri, huku akidai wataingia uwanjani kucheza kwa nguvu zote na kujitahidi kumiliki mpira kwa muda wote ili kuwanyima nafasi Prisons.

Kocha huyo raia wa Uingereza alidai kuwa amebaini kuwa wapinzani wake wanatumia nguvu sana, ikiwemo kubebwa na maumbile ya wachezaji wake ambayo ni makubwa na warefu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles