24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

YANGA HATIHATI KUMKOSA NGOMA

 

Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, timu ya Yanga, huenda wakamkosa tena mshambuliaji wao, Donald Ngoma, iwapo watashindwa kumjenga kisaikolojia ili kumsaidia kurejea kwenye kiwango chake cha kawaida.

Ngoma, ambaye alisajiliwa Yanga mwaka 2015, akitokea timu ya Platinum ya Zimbabwe, alikuwa akisumbuliwa na majeraha ya goti, yaliyomweka nje ya uwanja katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu msimu uliopita, ambapo alilazimika kwenda nchini Afrika Kusini kutibiwa.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Daktari wa Yanga, Edward Bavu, alisema  licha ya Ngoma kupona majeraha yake, bado hayupo  fiti asilimia 100, kutokana na kuathirika kisaikolojia na hali hiyo inaweza kumsababishia kupata majeraha mapya.

“Kuna mambo mengi yanaweza kusababisha mchezaji kama Ngoma asiweze kucheza katika kiwango chake bora, licha ya kupona majeraha yake.

“Majeraha ya muda mrefu yanaweza kumfanya mchezaji kuathirika kisaikolojia, na kama asipopata ushauri anaweza kupata majeraha wakati wowote anapokuwa uwanjani,” alisema Bavu.

Alisema kuwa, kuna athari nyingi anazopata mchezaji anapokuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu, ikiwamo kuongezeka uzito pamoja na kuongezeka kwa maji mwilini.

“Mabadiliko ya Yanga katika benchi la ufundi pamoja na kusajiliwa baadhi ya wachezaji wapya pia inaweza kuwa sababu nyingine inayowafanya baadhi ya wachezaji kushindwa kufanya vizuri kama ilivyo awali.

“Ni vema wachezaji hao wakapewa muda na kushauriwa kisaikolojia ili kuwasaidia kurejea kwenye uwezo wao wa kawaida,” alisema Bavu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles