28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

YALIYOMKUTA MESSI NA NEYMAR YAMKUTA NA ETO’O

BARCELONA, HISPANIA


samuel-etooBAADA ya mikasa na tuhuma za kukwepa kulipa kodi kuwaandama wachezaji wa timu ya Barcelona, Lionel Messi na Neymar Jr, sasa yamemkuta mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Samuel Eto’o.

Supastaa huyo wa Cameroon, ambaye alipata fursa ya kuzitumikia klabu za Real Madrid, Mallorca na Barcelona wakati akiwa nchini Hispania, sasa huenda akatupwa jela kwa miaka 10 kutokana na sababu za kukwepa kulipa kodi.

Kwa mujibu wa El Pais, Samuel Eto’o, mwenye umri wa miaka 35, ambaye anakipiga kwenye klabu ya Antalyaspor ya Uarabuni, huenda akatupwa jela miaka 10 pamoja na faini ya euro milioni 14 kwa hatia ya kukwepa kulipa kodi.

Sakata hilo la ukwepaji kodi linalomkabili Eto’o linahusishwa na kipindi cha kati ya mwaka 2006 hadi 2009, alipokuwa akiitumikia klabu ya FC Barcelona.

Mwaka 2006 Eto’o alicheza michezo 198 akiwa Barcelona, huku mwaka 2004 na  2009, akifunga mabao 129.

El Pais limeripoti namna Eto’o alivyomudu kukwepa kodi yenye thamani ya zaidi ya euro milioni 3.5.

Inasemekana Eto’o aliendesha kampuni mbili, moja ilikuwa Hispania Bulte 2002 na nyingine ilikuwa Hungary (Tradesport), zilizomwezesha kumiliki haki za matangazo ya kulipa kodi.

Eto’o pia anatuhumiwa kupokea mkwanja mrefu kutoka kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ya Puma bila kulipa kodi.

Inaaminika Puma ilikuwa ikimlipa Eto’o kati ya euro milioni 1.5 hadi milioni 3 kwa msimu.

Mkongwe huyo aliondoka Barcelona akiwa tayari amefanikiwa kutwaa Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili, huku Ligi Kuu ya Hispania akitwaa mara tatu, kabla ya kujiunga na timu ya Inter Milan ya Italia.

Eto’o pia aliwahi kucheza katika Ligi Kuu England katika timu ya Chelsea na Everton.

Julai mwaka huu, Lionel Messi akiwa na baba yake walihukumiwa kifungo cha miezi 21 jela kutokana na kosa la kushindwa kulipa kodi.

Licha ya Messi kutokwenda jela kutokana na kosa hilo lililokuwa la kwanza kwake kwa kigezo cha kifungo hicho kilikuwa chini ya miaka miwili, kwa mujibu wa sheria za nchi ya Hispania inamtaka mtenda kosa kusimamishwa kufanya shughuli zake Hispania.

Neymar na klabu ya Barcelona pia wanatarajia kukumbana na kisanga kama hicho kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles