27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

DIOUF ANOGESHA BIFU LAKE NA GERRARD

LONDON, ENGLAND


gerrard-hadjiPONGEZI nyingi zinaendelea kutolewa na wadau wa soka na wachezaji  kutoka kona zote za dunia, baada ya  Steven Gerrard kutangaza kutundika daluga.

Licha ya pongezi hizo kuwa chanya, mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, El-Hadji Diouf, ameendelea kumlalamikia nahodha huyo wa zamani wa England kwamba hana utu.

Straika huyo wa zamani wa Timu ya Taifa ya Senegal, ambaye anaingia katika vitabu vya historia ya Liverpool kuvaa jezi namba 9 kwa msimu mzima bila kufunga bao, ameendeleza vita ya maneno na Gerrard.

Diof na Gerald wamecheza kwa  pamoja kwa misimu miwili, wameendelea kuwa maadui  tangu  Msenegali huyo aliposajiliwa na  kocha Gerrard Houllier, kwa ada ya pauni milioni 10  Juni mwaka  2002.

Akihojiwa na runinga ya SFR nchini Ufaransa, Diouf amesema wakati anasajiliwa kwenda Liverpool, watu walimtahadharisha kuwa wapo baadhi ya wachezaji wasioguswa na iwapo utakwenda kinyume cha matakwa yao, utakuwa na wakati mgumu.

Ugomvi baina ya wachezaji hao ulitokana na kitabu alichoandika Gerrard akimuelezea Diouf kuwa hakujali soka wala klabu ya Liverpool.

Pamoja na kuyaita maelezo ya Gerrard  kuwa  ni ya kibinafsi, Diouf alisema alipowasili Anfield,  hakuwa tayari kumheshimu na aliwahi kumuuliza anakumbukwa kwa lipi katika michuano mikubwa kama ya kombe la Mataifa ya Ulaya na Kombe la Dunia, hivyo kwake yeye kiungo huyo si lolote.

“Namheshimu kama mchezaji, lakini kama binadamu mwenzangu hapana na nilishamueleza. Wapo waliokwenda kumweleza kocha niliyomweleza, akiwamo yeye na ndio tulipishana kauli,” alisema Diouf.

Diouf anasema: “Hakuweza kuniangalia usoni, alikuwa anaogopa hata kuzungumza na mimi. Tusisahau wakati nawasili sikuwahi kumuomba jezi, ila yeye aliomba jezi yangu ya Senegal kwa ajili ya rafiki yake.”

Wakati huo huo, Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, amesema milango ipo wazi kwa nahodha wa zamani wa klabu hiyo, Steven Gerrard, kurejea Anfield kama sehemu ya jopo la makocha wa klabu hiyo.

Inaelezwa kuwa, baada ya kutangaza kutundika daluga juzi, Gerrard, mwenye umri wa miaka 36, anaendelea na mazungumzo na uongozi wa klabu yake ya zamani ili kuwa kocha wa vijana.

Klopp amesema hivi karibuni watatangaza maamuzi waliyofikia baada ya mazungumzo kukamilika

“Nina hakika kwamba siku moja nitatangaza hatma ya suala hilo, lakini mpaka sasa sina la kusema. Milango ipo wazi kwake kwa upande wowote na nina uhakika ana matarajio hayo,” alisema Klopp.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles