27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, January 8, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Xavi ampa ushauri wa bure Guardiola

MANCHESTER, ENGLAND

KIUNGO bora wa zamani wa Barcelona, Xavi Hernandez, amempa ushauri wa bure kocha wake wa zamani Pep Guardiola ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha Manchester City, kuhamishia nguvu zake kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya hali kuwa mbaya kwenye Ligi Kuu England.

Manchester City ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England chini ya Guardiola, msimu huu wamekuwa kwenye wakati mgumu wa kutetea taji hilo na dalili zikionekana kuwa Liverpool wanaweza kutwaa ubingwa.

Liverpool ni vinara wakiwa na jumla ya pointi 55 baada ya kucheza michezo 19, huku Leicester City wakiwa nafasi ya pili kwa pointi 42 na Manchester City wakiwa na pointi 41 nafasi ya tatu, jambo ambalo ni ngumu kuweza kuwafikia Liverpool.

Xavi ambaye alikuwa na mafanikio makubwa chini ya Guardiola ndani ya Barcelona, lakini kwa sasa ni kocha wa klabu ya Al Sadd SC ya nchini Qatar, amemtaka Guardiola kutolea nguvu kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya badala ya Ligi Kuu England kwa kuwa wapo nyuma kwa pointi 14 dhidi ya Liverpool.

“Pep amezaliwa kuwa mshindi, najua inamuumiza sana kuachwa nyuma kiasi hicho dhidi ya Liverpool kwenye michuano ya Ligi Kuu England, lakini ninaamini bado hajakata tamaa.

“Ukweli ni kwamba, kwa nafasi aliyoachwa na Liverpool inaonesha wazi kuwa hawezi kufikia walipo wapinzani wake Liverpool na kisha kutetea ubingwa kwa mara ya tatu.

“Anakwenda kukutana na timu ya Real Madrid kwenye hatua ya 16 bora nyumbani na ugenini, hivyo ni vizuri kuwatengeneza wachezaji wake sasa kwa ajili ya michezo hiyo miwili migumu ambayo inaweza kumfanya abaki au ashindwe kuendelea na hatua inayofuata.

“Guardiola anapenda mataji, ninaamini kama angeulizwa mwanzo wa msimu kuwa nini anataka msimu huu ni Ligi ya Mabingwa kwa kuwa Ligi Kuu tayari amechukua mara mbili,” alisema Xavi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles