P Funk: Maprodyuza bado ni wachache

  0
  729

  GLORY MLAY

  MTAYARISHAJI wa nyimbo za wasanii wa bongo fleva, Paul Matthysse ‘P Funk’ amesema kwa sasa kuna watengenezaji wengi wa  midungo ‘beats’ na sio maprodyuza kama ilivyo zamani.

  Mtayarishaji huyo ambaye pia ni msanii, alizungumza na MTANZANIA jana, na kusema yeye anawaita ‘Beat Maker’ kutokana na kurahisishiwa mambo na utandawazi.

  “Teknolojia imekuwa na imerahisisha sana kazi, zamani tulikuwa tunatumia mifumo migumu, hivyo lazima uende studio na utayarishe kazi na inaweza kuchukua hata wiki moja, lakini kwa sasa mtu anatengenezea mdundo kwenye simu kisha anakwenda studio.

  “Ukifanya hivyo prodyuza hana kazi ya kufanya, ila kikubwa ni kuchkua ile na kisha kuichezea kidogo na kazi inakuwa imeisha, hivyo naweza kusema watengenezaji midundo ni wengi kuliko wazalishaji,” alisema.

  LEAVE A REPLY

  Please enter your comment!
  Please enter your name here