21.1 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Simba Vs Yanga ulinzi mara dufu

LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, amesema wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanaimarisha ulinzi wakati wa mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga itakayopigwa Jumamosi hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mambosasa aliwataka mashabiki na wapenzi wa mahasimu hao wa kabumbu nchini, kufika kwa wingi uwanjani hapo kwani kutakuwa na ulinzi wa uhakika.

“Aidha Jeshi la PolisI Kanda Maalum linawaasa mashabiki kushabikia kistaarabu na kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa sheria, hivyo basi hatutasita kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote atakayejaribu kufanya fujo,” alisema Mambosasa.

Simba wenye masikani yao Mtaa ya Msimbazi na Yanga inayotokea Twiga na Jangwani zinatarajiwa kushuka dimbani kuwania pointi tatu, ukiwa ni mwendelezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kabla ya mechi ya jana Simba ilikuwa imeshuka dimbani mara 12 na kujikusanyia pointi 31 baada ya kushinda mara 10, kutoka sare mara moja na kufungwa moja, huku watani wao Yanga, wakiwa wamecheza mechi 11, wakivuna pointi 24, wakishinda mara saba, sare tatu huku wakipoteza mechi moja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,592FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles