24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

WMA Mara yapiga tafu ujenzi wa Zahanati Butiama

Na Shomari Binda, Butiama

WAKALA wa Vipimo ( WMA) Mkoa wa Mara imechangia vifaa vya ujenzi kwa ajili ya Zahanati ya Kijiji cha Nyamikoma Kata ya Kyanyari wilayani Butiama.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo Kkjijini hapo, Diwani wa Kata ya Kyanyari, Mugingi Muhochi, amesema jambo walilofanya WMA linapaswa kuungwa mkono na kila mdau wa maendeleo katika kusaidia juhudi za Serikali.

Meneja wa Wajala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Mara, Muhono Nashon, (kulia)akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nyamikoma baada ya kutoa msaada wa vifaa vya ujenzi.

Amesema alipopeleka maombi kwenye taasisi hiyo ili kuchangia ujenzi wa zahanati hiyo hawakusita kuchangia sehemu ya ujenzi.

Muhochi amesema katika kipindi hiki wananchi wa kjiji cha Nyamikoma wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilometa 12 ili kutafuta huduma za afya na pale zahanati hiyo itakapokamilika itawasaidia.

Ameongeza kuwa vifaa walivyosaidia WMA ni sehemu ya kukamilisha ujenzi huo na kuwaomba wadau wengine pamoja na serikali kuunga mkono juhudi za wananchi ambao walianzisha ujenzi wa zahanati hiyo.

“Niwashukuru sana WMA kwa msaada wao ambao wametuletea siku ya leo ili kutusaidia kukamilisha zahanati ya hapa Nyamikoma itakayosaidia wananchi zaidi ya 80,000,”amesema Muhochi.

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Nyamikoma na viongozi wao wameshukuru Wakala wa Vipimo kwa msaada huo na kuwaomba wengine watakaoguswa kuweza kuwasaidia.

Kwa upande wake Meneja wa WMA mkoa wa Mara, Muhoni Nashon, amesema vifaa walivyotoa ni mbao na nondo vyenye thamani ya Sh milioni 2.5 kama sehemu ya ujenzi.

Amesema wamechangia kama wadau kwa kuunga mkono juhudi za serikali na kuwaomba wadau wengine kuchangia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles