24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Ilemela yafanikiwa kuwapanga machinga 3,187

Na Sheila Katikula, Mwanza

HALMASHAURI  ya Manisipaa ya Ilemela mkoani Mwanza imefanikiwa kuwapanga wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga  3,187 kwenye maeneo rasmi.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, Modest Apolinary kwenye kikao cha baraza la madiwani cha robo ya  kwanza cha julai-Septemba cha mwaka wa fedha 2021/2022.

Amesema kati ya wafanyabiashara hao wadogo kati yao wanaume ni 2345 na wanawake 842 ambao wote wametii kwa hiari kupelekwa kwenye masoko rasmi yaliyotengwa

“Tumewapeleka maeneo rasmi yaliyotengwa Nyasaka,Kirumba,Buzuruga,Nyamanoro,Pasiansia,Buswelu na Kitangiri kwani zoezi hili linafanyika sambamba na kuboresha miundo mbinu ya kuweka taa, maji,” amesema.

Naye Mkuu wa Wilaya hiyo, Hassan Masala amesema zoezi hilo limeliwa shirikishi hivo atakaye kutwa kwenye maeneo yasiyo rasmi anafanya biashara atachukuliwa sheria. 

Mbunge wa jimbo la Ilemela Dk. Angeline Mabula ameishauri halmashauri hiyo kujenga jengo la machinga complex ili kuondoa changamoto ya wafanyabiashara kukosa maeneo.

Diwani wa kata ya Ilemela, Willbard Kilenzi amewapongeza Mkurugenzi,Mkuu wa Wilaya kwa kufanya zoezi hilo kwa njia ya ushirkishi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles