WIZKID, BEYONCE, EMINEM JUKWAA MOJA

CALIFORNIA, MAREKANI


MKALI wa muziki nchini Nigeria, Wizkid, anatarajia kuuanza mwaka vizuri katika kazi zake za muziki baada ya kuthibitisha kuwa atapiga shoo jukwaa moja na Beyonce na Eminem.

Msanii huyo atafanya vitu vyake kwenye jukwaa la Muic and Arts Festival maarufu kwa jina la Coachella, tamasha hilo litaanza kufanyika Aprili 13 hadi 22, mwaka huu huko California, Marekani.

Tamasha hilo linafanyika kila mwaka mjini hapo huku wakikutanishwa mastaa ambao wanafanya vizuri duniani kwa kipindi hicho.

Wasanii wengine ambao watapiga shoo ni pamoja na rapa, Jidenna Mobisson kutoka Marekani, The Weeknd, Post Malone, Tyler The Creator, DJ Black Coffee kutoka Afrika Kusini na wengine wengi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here