24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

IDRIS NA MITANDAO YA KIJAMII HUMWAMBII KITU

NA JESSCA NANGAWE


MCHEKESHAJI maarufu hapa nchini, Idris Sultan, amesema hawezi kukaa mbali na mitandao ya kijamii kwani licha ya kuwa ni sehemu ya kujiongezea mashabiki, lakini pia imekua ikimpatia dili mbalimbali na kumwongezea kipato.

Idris ambaye pia alikua mshindi wa shindano la Big Brother Africa 2014, alisema kutokana na maisha ya sasa kuhitaji utandawazi zaidi amejikuta akitegemea mitandao ya kijamii katika kuendesha kazi zake na kupata mipango mingi ya kumwingizia fedha.

Akizungumza na MTANZANIA, alisema mara zote amekua akishinda kwenye  mitandao ya kijamii si kwa ajili ya kujifurahisha kwani ameendelea kukutana na watu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania ambao wanatamani kufanya naye kazi.

“Wengine wanadhani hii mitandao tunashiriki kwa kujifurahisha tu, wengine ndio kama ofisi, tunaitumia kuingiza kipato, nimekua nikipata dili mbalimbali kwa kukutana na watu kwenye mitandao, nimekua nikiifanya kama ofisi yangu binafsi,” alisema Idris.

Sultan mbali na kufanya matangazo pia anafanya biashara ya kuuza viatu vyake vinavyojulikana kwa jina la Sultan Xforemen.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles