27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

WIZI WA NYWELE WAKITHIRI NCHINI INDIA

NEW DELHI, INDIA

HALI ya wasiwasi imetanda katika baadhi ya majimbo nchini India kutokana na wizi wa nywele kuongezeka, hali inayowatatiza zaidi wanawake.

Wanawake zaidi ya 50 kutoka majimbo ya Haryana na Rajasthan yaliyoko Kaskazini mwa India wamejitokeza kulalamika kukatwa nywele zao wakati wakiwa wamepoteza fahamu.

Hata hivyo, maafisa wa polisi nchini humo wanajaribu kuchunguza suala hilo, ambalo limewaacha wanawake wakiwa na masikitiko makubwa kupoteza nywele zao.

Nywele zinathaminiwa na wanawake kwa vile hutumika katika kujirembe na kuwa na mvuto wa kipekee.

“Kulikuwa na mwanga mkali uliosababisha nipoteze fahamu. Saa moja baadaye niligundua kuwa nywele zangu pia zimekatwa,” alisema Sunita Devi, mwanamke mwenye umri wa miaka 53 kutoka Haryana.

Akaongeza: “Nimeshindwa kulala wala kufanya chochote. Nilisoma kuhusu visa hivi vikifanyika huko Rajasthan, lakini sikufikiria vingenitokea,” anasema.

Naye Asha Devi alipoteza nywele yake katika kisa kama hicho siku iliyofuata.

Baba mkwe wake, Suraj Pal anasema kutokana na kisa hicho, alimshauri akiwa na wanawake wengine wa familia kuhamia nyumba ya jamaa wao katika jimbo la Uttar Pradesh.

Aidha Pal amesema alikuwa nyumbani wakati Asha Devi akitoka nje kufanya kazi zake.

“Nilienda nje kujua ni kwa nini hakurudi baada ya zaidi ya dakika 30. Tulikuta amepoteza fahamu bafuni. Nywele zake zilikuwa zimekatwa na kutupwa sakafuni.”alisema.

Ripoti za kunyolewa wanawake kwanza ziliibuka mapema Julai mwaka huu katika Jimbo la Rajasthan ikishuhudia wizi wa kwanza wa nywele, kisha visa vikaenea katika jimbo la Haryan na mji mkuu Delhi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles