29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 9, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS OBASANJO AOMBA KUMTEMBELEA JELA KIONGOZI WA UPINZANI ZAMBIA

LUSAKA, ZAMBIA

RAIS wa Zambia Edgar Lungu juzi alifanya mazungumzo na Rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo, ambaye aliomba kuruhusiwa kumtembelea kiongozi wa upinzani aliye jela.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Rais, Amos Chanda, viongozi hao wawili pamoja na mambo mengine walizungumzia juhudi za Obasanjo za kuhamasisha amani pamoja na kampeni yake ya kupambana na polio barani Afrika.

Chanda alisema kiongozi huyo wa Nigeria aliyemtembelea Rais Lungu Ikulu ya hapa pia aliomba kumtembelea kiongozi wa upinzani Hakainde Hichilema.

Hichilema yuko kizuizini tangu Aprili mwaka huu akikabiliwa na mashitaka ya uhaini.

Chanda alisema Rais Lungu amekubali ombi hilo la Obasanjo kumtembelea kiongozi huyo katika gereza lenye ulinzi mkali la Mukobeko, kilomita 150 kaskazini mwa Lusaka.

Lungu pia aliliagiza Jeshi la Anga la Zambia kumpeleka Obasanjo gerezani.

Mwezi uliopita Rais Lungu alitangaza hali ya dharura ili kukabiliana na kile alichoita vitendo vya hujuma vinavyofanywa na mahasimu wake wa kisiasa, baada ya moto kuteketeza soko kubwa nchini humo.

Rais Lungu alimshinda Hichilema kwa ushindi mwembemba katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2016, ambao upinzani umedai kujaa wizi na udanganyifu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles