26.6 C
Dar es Salaam
Saturday, December 3, 2022

Contact us: [email protected]

CHINA YAITAKA KOREA KASKAZINI KUSITISHA MAJARIBIO YA MAKOMBORA

BEIJING, CHINA

SERIKALI ya China imeitaka Korea Kaskazini kusitisha majaribio ya makombora baada ya vikwazo vipya vilivyowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC).

Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi, alimshauri waziri mwenzake wa Korea Kaskazini, Ri Yong-ho kuheshimu maazimio ya Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano wao uliofanyika nchini Philippines.

Hata hivyo hakusema majibu aliyotoa Ri.

Siku ya Jumamosi UNSC lilichukua hatua madhubuti ya kuiadhibu Korea Kaskazini kwa hatua yake ya mwezi uliopita ya kufanyia majaribio zana zake za nyuklia.

Katika kura ya pamoja, baraza hilo liliidhinisha vikwazo vipya vinavyolenga biashara ya chuma na makaa ya mawe, ambayo Pyongyang huuza nje bidhaa hizo kwa zaidi ya dola bilioni kwa mwaka.

Rais wa Marekani Donald Trump, alipongeza hatua za China na Urusi za kuunga mkono vikwazo hivyo vilivyotolewa na UNSC.

Anasema kuwa, vikwazo hivyo, vitakuwa na ‘athari kubwa mno’ ya kibiashara kwa Korea Kaskazini.

Majirani wao Korea Kusini, wameiomba Korea Kaskazini kufuata njia ya mazungumzo, ili kutanzua mzozo uliopo wa mpango wa Pyongyang kuhusu zana za nyuklia.

Beijing pia inaomba kurejelewa kwa mazungumzo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,532FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles