24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

Wizara ya Nishati na Madini yang’ara kimataifa

Pg 2Na Teresia Mhagama

WIZARA ya Nishati na Madini, imepata tuzo ya ki¬mataifa ya mwaka ya Maendeleo ya Udhibiti wa sekta ndogo ya mafuta na gesi.

Tuzo hiyo ya mwaka 2014 inayotolewa na Kampuni ya Kimataifa ya Wildcat International ya nchini Marekani kupitia machapisho yake maarufu duniani ya The Oil & Gas Year (TO&GY), imekabidhiwa rasmi mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam kwa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene kwa niaba ya wizara hiyo.

Tuzo hiyo iliyotolewa na Mratibu wa Mahusiano kwa Wateja kutoka Jarida la TO&GY, Laura Carr, inaitambua wizara hiyo kutokana na mafan¬ikio yake katika kushughulikia changamoto za udhibiti wa sekta ndogo ya mafuta na gesi na hivyo kuchochea maende¬leo ya sekta hiyo.

Mafanikio hayo ni pamoja na kuwa na sera mpya ya gesi asilia, kuwa na muundo mpya wa makubaliano ya gharama za utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi na kuwa na rasimu ya sera ya uweze¬shaji na ushirikishaji wazawa.

“Hayo ni baadhi tu ya maendeleo yaliyoifanya sekta hii kueleweka na kuku-balika zaidi kwa wawekezaji na wadau,” inasomeka sehemu ya maandishi yaliyoko katika Jarida la TO&GY.

Pamoja na tuzo ya wiz¬ara iliyotolewa na T0&GY, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kupitia kwa Mkurugenzi wake, Mhandisi Felchesmi Mramba, ameshinda tuzo ya mtu wa mwaka kutoka-na na mipango yake ya Dola za Marekani bilioni sita zitakazowezesha Tanesco kuongeza uzalishaji umeme mara tatu zaidi ya sasa kutokana na uwepo wa vyanzo mbalimbali vya umeme.

Wakati hayo yakiendelea, Shirika la Maende¬leo ya Petroli Tanzania (TPDC), limeshinda tuzo iitwayo transition of the year (2014) kutokana na kupiga hatua katika shughuli zake.

Mbali ya kuwa mdhibiti wa sekta ndo¬go ya mafuta na gesi nchini, TPDC limekuwa mwekezaji baada ya kushinda tenda na kupata vitalu viwili kwa ajili ya utafiti wa mafuta na gesi nchini.

Usambazaji wa machap¬isho ya TO&GY hukaguliwa na Taasisi ya Marekani ya BPA Worldwide, inayokagua machapisho maalumu zaidi ya 2,600 katika nchi 30 duniani yakiwamo majarida maarufu ya Toronto Star, Wall Street Journal na Gulf News.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles