26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Membe: China ni marafiki zetu wa ukweli

zimbabwenew1Na Ruth Mnkeni, Dar es Salaam
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema Serikali ya China ni marafiki wa uhakika kwa kuwa wameisaidia Tanzania kufungua idara maalumu ya upasuaji wa ugonjwa wa moyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mbali na hilo, Waziri Membe amesema kuwa Serikali ya nchi hiyo, imesaidiana kwa kiasi kikubwa na nchi za Afrika Mashariki katika kutatua migogoro na vita vya wenyewe kwa wenyewe katika baadhi ya nchi hizo.
Akizungumza juzi usiku wakati wa sherehe za mwaka mpya wa China, Waziri Membe alisema kitendo cha Serikali ya China kuisaidia Tanzania katika sekta ya afya, ni chachu ya maendeleo kwani wagonjwa wa moyo watakuwa wakitibiwa nchini.
“Serikali ya China imeona umuhimu wa sekta ya afya nchini ndiyo maana imeona ni vema ikatusaidia kufungua kitengo maalumu cha upasauaji wa ugonjwa wa moyo na hii itatufanya sasa tuanze kuwatibu hapa nchini wagonjwa wa moyo badala ya kuwapeleka nje ya nchi.

“Kwa kifupi China ni marafiki zetu, wako tayari kutusaidia mara zote na wamekuwa wakionyesha kuguswa na shida zetu ndiyo maana nasema hawa wenzetu ni marafiki wa kweli na wana nia njema na sisi,” alisema Membe.
Pamoja na hayo, alisema ushirikiano kati ya Tanzania na China, umejengeka katika nyanja zote zikiwamo kisiasa, kijamii na kiuchumi.
Akizungumzia sherehe hizo, alisema Wachina wana kawaida ya kuipa majina miaka na kwamba mwaka jana walikuwa wanatumia jina la farasi na mwaka huu walitumia jina la kondoo wakimaanisha amani na usalama katika nchi husika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles