25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wizara, Mikoa zatakiwa kuondoa vikwazo ujenzi wa viwanda

                           Na Mwandishi Wetu

Wizara zinazohusika na masuala ya viwanda, Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja na sekta binafsi zimetakiwa kutambua na kuondoa vikwazo na urasimu dhidi ya ujenzi na ustawi wa viwanda nchini.

Agizo hilo limetolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Jumamosi Novemba 3, wakati akifunga wiki ya maonesho ya viwanda yaliyofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba katika kata ya Picha ya Ndege, Kibaha mkoani Pwani ambapo amesema uwepo wa viwanda nchini unatoa ajira nyingi.

Pia, Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage ampelekee taarifa ya hatua iliyofikiwa juu ya kampuni ya Budget Motors walioomba kibali cha kutengeneza na kuunganisha bodi za mabasi tangu mwaka jana na hawajajibiwa.

“Serikali ya imeamua kujenga uchumi wa viwanda utakaokuwa mhimili mkuu wa maendeleo ya Taifa na wananchi, hivyo itaendelea kutoa ushirikiano ili kuhakikisha ajenda ya ujenzi wa viwanda inafanikiwa, katika kupunguza vikwazo na kuboresha sera nchini imeweka msukumo wa kutosha ili kuondoa ukiritimba kwenye shughuli zote za kibiashara, lakini pia katika kuboresha sera za Taifa za kodi ili kulinda viwanda vya ndani, “amesema.

Amesema Rais Dk. John  Magufuli alitoa msukumo wa sekta binafsi nchini kuanzisha viwanda vinavyotumia malighafi zinazozalishwa nchini kutokana na mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na maliasili, vikiwemo viwanda vya nguo, sabuni, korosho na matunda.

“Uwepo wa viwanda nchini utasaidia kuongeza wigo wa mapato ya Serikali kupitia kodi na tozo mbalimbali, huu ndio mwelekeo wa Serikali ya awamu ya tano unaolenga kuifikisha nchi kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025,” amesema Majaliwa.

Kuhusu suala la kampuni ya Budget Motors, Waziri Mkuu amesema ifikapo Ijimaa Novemba 9, Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji awasilishe taarifa kuhusu suala hilo la kibali na amesema ni bora apewe atengeneze na akikosea arekebishwe.

Kampuni ya Budget Motors inadai kuwa iliomba kibali cha kuwa na uthibitisho wa kutengeneza na kuunganisha bodi za mabasi kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS), kwa takribani mwaka mmoja bila ya kujibiwa. Walitoa malalamiko hayo kwa Waziri Mkuu alipotembelea banda lao.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles