MSANII Witness Mwaijage amesema ameamua kuunda kundi la wasanii wanaoimba muziki wa hip hop alilolipa jina ‘Female Lapaz Empowerment’ ili wasaidie kukuza muziki huo kwa wanawake.
“Tumeamua kuungana ili wasanii wa kike hasa wanaorap wapate mafunzo na kuiga kwetu namna ya kudumu katika muziki huo kwa muda mrefu tofauti na sasa,’’ alisema Witness.
Kundi hilo lilianzishwa likiwa na wasanii 11 na kwa sasa wapo 17, wasanii wengine ni Chemical, Sindi, Kitifa na Sister P.