MSIMAMIZI wa mashindano ya Urembo Tanzania, ‘Miss Tanzania’, Hashimu Lundenga, ametambulisha kamati mpya ya muda inayoundwa na wajumbe 12 akiwemo Jokate Mwegelo aliyekuwa Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006.
Mwenyekiti wa kamati hiyo ni Juma Pinto, makamu mwenyekiti, Lucas Ritta, katibu mkuu ni Doris Mollel na Joketi Mwegelo ambaye ndiye anakuwa msemaji wa kamati hiyo.
Wajumbe wengine ni Hoyce Temu, Mohamed Bawazir, Gladyz Shao, Magdalena Munisi, Shah Ramadhani, Hamm Hashim, Khalfan Saleh na Ojambi Masaburi.
Lundega alidai ameunda kamati hiyo ili kubadilisha mwonekano mpya wa wajumbe katika shindano hilo kwa mwaka huu.