29.9 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

NURU THE LIGHT: Hakuna tatizo msanii kushabikia chama cha siasa

Nuru the LighttNA JULIET MORI, (Tudarco)
MSANII wa Bongo Fleva anayefanyia shughuli zake za kimuziki nchini Sweeden, Nuru Magram ‘Nuru the Light’, amesema haoni ubaya kwa wasanii kuweka wazi ushabiki wao kwenye vyama vya siasa kwa kuwa kila mtu ana chama anachokipenda.
Nuru aliweka wazi hilo jana baada ya kutumbuiza na wafanyakazi wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd ikiwa ni ishara ya kukubali mchango wa kazi zinazofanywa na wafanyakazi wa kampuni hiyo kupitia magazeti yake matano ya Mtanzania, Bingwa, Dimba, The African na Rai.
Nuru aliimba nyimbo mbalimbali za zamani na mpya ukiwemo ‘Chapalapa’, ‘Usilale Nakuja’, ‘Muhogo andazi’ na, ‘L’
unaowakilisha ‘Light’, ‘Love’ na ‘Life’.
“Nimefurahi kujumuika nanyi leo (jana) na pia kwa kuwa mmefurahia muziki wangu kiasi cha kuwa tayari niwaletee CD za nyimbo zangu nilizotombuiza hapa, naamini tutaendelea kushirikiana katika kazi zetu kwa kuwa wasanii tunategemeana nanyi waandishi na wafanyakazi wote wa masuala ya habari,’’ alieleza Nuru.
Katika hatua nyingine, Nuru ameongeza kuwa anafurahishwa na hamasa waliyonayo Watanzania katika masuala ya siasa hasa kuelekea uchaguzi wa Oktoba.
“Uchaguzi wa mwaka huu hautabiriki, una upinzani mkubwa na watu wengi wameshajiandikisha kwenye daftari la
kudumu na wana hamasa ya kupiga kura kuchagua viongozi wanaowataka hivyo hata wasanii tuna fursa ya kuonyesha tunakopenda,’’ alisema Nuru.
Pia alisisitiza kwa kuwataka watu wasishawishike na zawadi ndogo ndogo watakazopewa na baadhi ya wanasiasa ili

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles