26.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Winga Azam aitaka timu ya beki wa Arsenal

FARIDNA ZAINAB IDDY, DAR ES SALAAM

WINGA wa timu ya Azam FC, Farid Mussa ambaye yuko katika majaribio nchini Hispania, ameweka wazi kuwa malengo yake ni kucheza katika klabu ya Malaga aliyowahi kuitumikia beki wa Arsenal, Nacho Monreal.

Farid alianza majaribio rasmi Hispania Jumatatu iliyopita akiwa na kikosi cha timu ya CD Tenerife inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini humo, kabla ya wiki ijayo kuendelea na majaribo katika timu za Las Palmas na kumalizia Malaga.

Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi kutoka Hispania, Farid alisema kuwa licha ya kuwa na uhakika wa kufanya majaribio katika timu hizo tatu, lakini lengo lake ni kupata nafasi ya kuwa moja ya wachezaji katika kikosi cha Malaga.

“Wakala wangu John Sorzano raia wa Venezuela, amenihakikishia kufanya majaribio katika timu hizo tatu huku nikianza na CD Tenerife kisha hizo nyingine, lakini binafsi lengo na furaha yangu ni kupata nafasi kwenye kikosi cha Malaga kinachoshiriki Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’, ambacho naamini kitanifikisha mbali kisoka.

Nyota huyo chipukizi aliyekuzwa na kituo cha kulea vipaji cha Azam FC, atakuwa nchini Hispania kwa takribani wiki tatu na anatarajia kurejea nchini Mei 19 mwaka huu.

Iwapo atafuzu katika majaribio hayo, atakuwa Mtanzania wa kwanza kucheza katika klabu kubwa nchini Hispania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles