33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Vita ya vigogo uchaguzi Yanga  

TARIMBANA ZAINAB IDDY, DAR ES SALAAM

WAKATI vuguvugu la uchaguzi mkuu wa Klabu ya Yanga likionekana kufukuta chini kwa chini, aliyewahi kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Abasi Tarimba, anadaiwa kuwa miongoni mwa watakaowania nafasi ya uenyekiti kwa mara nyingine.

Tarimba ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), aliwahi kuiongoza Yanga kwa mafanikio mwanzoni mwa miaka ya 2000.

Taarifa ambazo MTANZANIA Jumamosi limezipata kutoka kwa baadhi ya wanachama wenye nafasi kubwa ndani ya Yanga, zinasema hivi sasa wapo katika mchakato wa kuhakikisha wanamshawishi Tarimba ili aweze kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo ya juu ndani ya klabu hiyo.

“Tarimba anastahili kurejea Yanga ili aweze kuiongoza kwani kwa kipindi cha hivi karibuni kumekuwa na migogoro mingi inayoendelea ndani kwa ndani ambayo kipindi alichokuwepo haikujitokeza.

“Mimi (anataja jina) na wenzangu hivi sasa tupo kwenye mchakato wa kumshawishi Tarimba akachukue fomu ya kuwania uenyekiti na tunaamni kwa kuwa ni muelewa na anapenda maendeleo ya Yanga, atafanya hivyo,” alisema.

MTANZANIA Jumamosi lilimtafuta Tarimba ambaye alisema kuwa kwa sasa bado mapema mno kuzungumzia jambo hilo ingawa kama mwana-Yanga ana haki yake kikatiba.

“Ni mapema mno kusema nitagombea maana zoezi la uchukuaji fomu kwa mujibu wa kamati inayosimamia uchaguzi huo litatangazwa Mei 3 mwaka huu, hivyo tusubiri muda ukifika itajulikana,” alisema.

Mbali na Tarimba, wapo pia wanaotajwa kuwania nafasi hiyo kuwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Usajili wa Yanga, Abdallah Bin Kleb huku Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete akitajwa katika nafasi hiyo.

Yanga wamelazimika kufanya uchaguzi huo baada ya hivi karibuni Baraza la Michezo Taifa (BMT), kutoa siku 72 kwa TFF kuhakikisha wanasimamia uchaguzi mkuu wa Wanajangwani hao kutokana na kushindwa kufanyika kwa kipindi cha miaka miwili sasa.

Kufuatia agizo hilo la BMT, TFF kupitia kamati yake ya usajili iliyopo chini ya wakili Aloyce Komba, ilitangaza Mei 5 mwaka huu kuwa utafanyika uchaguzi huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles