20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga mwendo wa dozi  

yanga kikosiNA ZAINAB IDDY, DAR ES SALAAM

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, timu ya Yanga leo itakuwa kibaruani katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kucheza na Toto Africans.

Tayari kocha mkuu wa timu hiyo, Hans van Pluijm, amesema kuwa kwa sasa ni mwendo wa kugawa dozi kwa kila timu watakayokutana nayo ili kutwaa ubingwa huo.

“Kikubwa kwa sasa hivi ni ushindi tu, tunahitaji ushindi ili kuweza kutimiza malengo yetu ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu,” alisema Pluijm.

Yanga ambayo inaonekana kutaka kutetea ubingwa huo, kwa hivi sasa inaongoza ligi ikiwa na pointi 62 baada ya kucheza mechi 25, ambapo wameshinda mechi 18, sare tano huku ikipoteza mechi moja pekee.

Kikosi hicho kinaingia kwenye mchezo huo huku kikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 2-1 Jumatano dhidi ya Mgambo Shooting katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa upande wa Toto Africans walio chini ya kocha John Tegete, wao wapo nafasi ya 11 wakiwa na pointi 30 baada ya kucheza mechi 27 ambazo wamepata sare tisa, kushinda mara saba na kupoteza michezo 11 hadi sasa.

Kikosi hicho kinaingia uwanjani kikiwa kimetoka kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Aprili 17 mwaka huu.

Licha ya kutokuwa na hasara yoyote iwapo watapoteza mchezo huo baada ya kujihakikishia kusalia kwenye ligi msimu ujao, lakini Toto inahitaji matokeo ya ushindi ili iweze kujiweka kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Mbali na mechi hiyo, michezo mingine itakayochezwa leo ni kati ya Mwadui dhidi ya Stand United katika Uwanja wa Mwadui Complex, Mtibwa Sugar wataikaribisha Mbeya City, huku Tanzania Prisons wakiikaribisha JKT Ruvu katika Uwanja wa  Sokoine Mbeya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles