27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wenger bado ajipa matumaini ya ubingwa

FBL-ENG-PR-NEWCASTLE-ARSENALLIVERPOOL, ENGLAND

BAADA ya klabu ya Arsenal kutoa sare ya 3-3 dhidi ya Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu nchini England, kocha wa klabu hiyo, Arsene Wenger, amedai bado ana nafasi ya kuchukua ubingwa msimu huu.

Wenger amesema ni bora kutoa sare kuliko kufungwa, kwa kuwa sare bado inakupa pointi, hivyo bado ana kila sababu ya kudai kwamba anaweza kuchukua ubingwa msimu huu.

“Nimechanganywa na matokeo dhidi ya Liverpool, lakini sijachukia kiwango ambacho wamekionesha wachezaji wangu, ni wazi kwamba walionesha uwezo wa hali ya juu huku wakiwa nyuma kwa mabao lakini walifanikiwa kuyarudisha.

“Lakini kwa matokeo kama haya dhidi ya timu kubwa kama Liverpool bado nina nafasi ya kusema kuwa msimu huu nitafanikiwa kuchukua ubingwa.

“Kama tutaendelea kucheza soka la hali hii basi hatuna wasi wasi na michezo ambayo ipo mbele yetu kwa sasa,” alisema Wenger.

Hata hivyo, kocha huyo alidai kwamba alishuka dimbani hapo huku akiwa na kumbukumbu mbaya ya kipigo ambacho alikipata mwaka 2014 cha mabao 5-1.

“Timu yangu ilikuwa inacheza huku ikiwa na kumbukumbu ya kichapo cha mabao 5-1 ya mwaka 2014, lakini hiyo ilikuwa zamani sasa tupo katika ubora mwingine,” aliongeza.

Timu hiyo kwa sasa bado inaongoza ligi nchini England ikiwa na pointi 43 baada ya kucheza michezo 21, ikiwa sawa na Leicester City lakini wakitofautiana kwa idadi ya mabao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles