ALIYEKUWA kocha wa Real Madrid, Rafa Benitez, ameibukia katika Uwanja wa Anfield kwa ajili ya kuangalia mchezo wa Ligi Kuu nchini England kati ya Liverpool dhidi ya Arsenal.
Katika mchezo huo ambao ulivuta hisia za mashabiki wengi duniani, lakini ulimalizaka timu hizo zikitoka sare ya 3-3.
Kwa mara ya kwanza kocha huyo ameonekana uwanjani tangu afukuzwe na uongozi wa Madrid wiki iliyopita, hata hivyo kocha huyo aliwahi kuifundisha klabu ya Liverpool kuanzia mwaka 2004 hadi 2010.
Katika kipindi anaifundisha klabu hiyo alifanikiwa kuchukua taji la Ligi ya Mabingwa na Kombe la FA. Lakini kwa sasa anaamua kupumzika kwa muda mara baada ya kuachwa na Madrid.
Klabu ya Madrid ikiwa chini ya kocha mpya, Zinedine Zidane, imeanza vizuri kwa kupata ushindi wa kwanza wa kishindo wa mabao 5-0 dhidi ya Deportivo.