30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Van Gaal matatani mwishoni mwa wiki hii

van-gaal-man-united-christmasMANCHESTER, ENGLAND

KLABU ya Manchester United inaweza kumfungashia virago kocha Van Gaal endapo ataupoteza mchezo wake dhidi ya Liverpool kwenye Uwanja wa Anfield.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 64, alikuwa na wakati mgumu mwezi uliopita ambapo alipewa michezo miwili ya kulinda kibarua chake, hata hivyo uongozi wa klabu hiyo uliendelea kumpa muda.

Lakini kuna taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zimelifikia Gazeti la The Times, zinasema kwamba uongozi huo umeanza kufanya mazungumzo na aliyekuwa kocha wa Chelsea, Jose Mourinho, kuweza kuchukua nafasi ya Van Gaal.

Hali hiyo inaonekana wazi kwamba atakuwa na wakati mgumu endapo ataupoteza mchezo wake wa mwishoni mwa wiki hii dhidi ya Liverpool, ambapo Manchester United itakuwa ugenini.

Mchezo uliopita wa Ligi Kuu, Manchester ilishuka dimbani dhidi ya Newcastle lakini mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 3-3.

Kwa sasa Manchester United inashika nafasi ya sita katika msimamo wa ligi, lakini viongozi wa klabu hiyo wamechoshwa na mwenendo wa klabu hiyo hivyo wako mbioni kumfungashia virago kocha huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles