20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Alade athibitisha kutoka na Bien

Yemi-AladeABUJA, Nigeria

NYOTA wa muziki kutoka nchini Nigeria, Yemi Alade, amethibitisha kuwa anatoka kimapenzi na mmoja wa wasanii ambao wanaunda Kundi la Sauti Sol, Bien Baraza.

Wasanii hao walikutana nchini Kenya kwenye msimu huu wa Coke Studio, ambapo jumla ya wasanii 28 kutoka Uganda, Kenya, Tanzania, Msumbiji na Nigeria walikutana kwa ajili ya kufanya kazi pamoja za Coke.

Hapo ndipo uhusiano wa Yemi na Bien ulipoanza, lakini Yemi ameweka wazi baada ya msanii huyo kutokana nchini Kenya kumuandikia wimbo wake wa ‘No Gode’ kwa Kiswahili, ambapo Yemi aliuandika kwa Kiingereza.

“Nakupenda sana mpenzi wangu Bien, umetoa mchango mkubwa katika kazi yangu mpya kwa kuifanya iwe kwa Kiswahili na ulitumia muda wako kufanya hivyo, nitaendelea kukupenda daima,” aliandika Yemi kwenye mtandao wa  Instagram.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles