27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Wenger aguswa na kiwango cha Alex Iwobi

Arsenal Training SessionLONDON, ENGLAND

NYOTA wa klabu ya Arsenal na timu ya Taifa ya Nigeria, Alex Iwobi, amezidi kumgusa kocha wake, Arsene Wenger, baada ya kupachika bao moja katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Watford.

Mchezaji huyo alianza kuonesha ubora wake wa kupachika mabao katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Everton Machi 19 mwaka huu katika ushindi wa mabao 2-0, huku mchezaji huyo akipachika bao moja, lakini mchezo wa juzi alitikisa nyavu na kumfanya kocha Wenger aguswe na uwezo wake.

Wenger amesema kwamba, mchezaji huyo atakuja kuwa na ubora zaidi kutokana na kile anachokifanya kwa sasa katika kila mchezo ambao anapewa nafasi.

“Kutokana na umri wake ninaamini Iwobi bado ana nafasi ya kuonesha uwezo wake, anaonesha kujiamini kwa kiasi kikubwa hivyo ninajivunia kuwa na mchezaji chipukizi mwenye uwezo wa hali ya juu.

“Ataendelea kupewa nafasi kutokana na kile ambacho anakifanya, tunahitaji wachezaji wenye uwezo na kujituma kwa ajili ya timu,” alisema Wenger.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles